23 Juni 2019 - 04:17
Baada ya vitisho vya Answarullah, Imarati yaondoa vifaru vyake kusini mwa Yemen

Habari kutoka nchini Yemen zinasema kuwa, Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) ambayo ni mmoja wa wavamizi wakuu wa ardhi ya Yemen umeondoa vifaru vyake 20 katika mji wa Aden wa kuisni mwa Yemen.

(ABNA24.com) Habari kutoka nchini Yemen zinasema kuwa, Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) ambayo ni mmoja wa wavamizi wakuu wa ardhi ya Yemen umeondoa vifaru vyake 20 katika mji wa Aden wa kuisni mwa Yemen.

Hatua hiyo ya Imarati imechukuliwa baada ya Nasruddin Amir, Kaimu Waziri wa Habari wa Yemen kuonya siku ya Jumanne kwamba iwapo Umoja wa Falme za Kiarabu utaendeleza vita nchini Yemen, basi viwanja vyake vya ndege na bandari zake zitakuwa shabaha ya makombora ya Jeshi na Kamati za Kujitolea za Wananchi wa Yemen.

Gazeti la "Aden al Ghad" la Mansour Hadi, rais wa zamani wa Yemen aliyejiuzulu na kukimbilia Saudi Arabia limeandika kuwa, meli moja ya Imarati ya kubeba vifaru ilifika katika mji wa bandari wa Aden baada ya udhibiti wa mji huo kutoka mikononi mwa serikali ya wokovu wa kitaifa ya nchi hiyo, lakini Ijumaa ya tarehe 21 Juni 2019 vifaru 20 vya Imarati viliondoka mjini humo. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, upande vinakoelekea vifaru hivyo haujulikani ingawa baadhi ya watu wanaamini kuwa vinaelekea upande wa kisiwa cha Āssab nchini Eritrea.

Huku hayo yakiripotiwa, msemaji wa majeshi ya Yemen amesema kuwa, harakati ya Answarullah ina teknolojia ya kisasai kabisa ambayo ni vigumu kugunduliwa na mifumo ya ugunduzi duniani.  Televisheni ya al Mayadeen imemnukuu Yahya Saree akiashiria namna mifumo ya ugunduzi ya Marekani inavyoshindwa kugundua droni na makombora ya Yemen yanayopiga kila siku huko Saudi Arabia na kusema kuwa, makombora na droni zote za Yemen hupiga kwa mafanikio maeneo yaliyokusudiwa.

Kwa upande wake, televisheni ya al Alam imetangaza kuwa, jeshi la Yemen na harakati ya Answarullah wamefanikiwa kuiteka kambi ya kijeshi ya al Qais iliyokuwa inatumiwa na mamluki wa Saudi Arabia huko Jizan, kusini mwa Saudia.



/129